Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara Fomu ya Mrejesho

Tovuti ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Kuhusu Muungano

Waasisi walibadilishana Kanuni a Misingi za Muungano na kuchanganya udongo wa Tanganyika na ule wa kutoka Zanzibar kuwa ni ishara ya muungano wan chi mbili. Mheshimiwa Mwalimu Julius Kambarage alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania. Mheshimiwa Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais, na Mzee Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kanuni za Msingi za Muungano wa mwaka 1964 zinaeleza kwamba chimbuko la Muungano , pamoja na mambo mengine linajumuisha uhusiano wa karibu wa muda mrefu kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar, uhusiano wa kisiasa uliotokana na harakati za kupigania uhuru zinazofanan na imani ya pamoja ya Uhuru wa Afrika yote. Kwa hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Bara la Afrika imewezekana kuunganga kwa mataifa mawili huru yanayojitawala. Tukio hili limeonyesha kwamba kuwa na dhamira ya dhati na kuwa na ari na moyo kwa watu wa Afrika na viongozi wao, inawezekana kuwa na umoja wa Afrika. Imedhihirika kuwa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ndiyo umoja pekee ambao bado unaendelea miongoni mwa miungao adimu sana duniani kote. 

Matukio yajayo

22

Mar

Fainali za Mashindano ya Tamasha la Muziki.

24

Apr

Fainali za Kombe la Muungano

25

Apr

Mkesha wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

26

Apr

Sherehe za Kilele cha Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar