Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara Fomu ya Mrejesho

Tovuti ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Sera ya Faragha

Tamko hili kuhusu faragha linatumika kwa Tovuti ya Muungano na vyombo vingine vyoyote vya kisheria vinavyodhibiti, kuhakiki au kutumia taarifa zitakazochukuliwa kupitia Tovuti hii bila ya kutoa taarifa yoyote ya binafsi. Hata hivyo mtumiaji, unakubali kutumia taarifa hiyo  kwa mujibu wa tamko hili la Sera.

Tafadhali zingatia kuwa Tovuti hii ina viungo vya kwenye tovuti nyingine, visivyotawaliwa na tamko hili la faragha.

Iwapo una swali au kero yoyote kuhusu tamko hili la faragha, tumia kiungo cha “maoni” au tuma barua pepe. Tovuti hii haitachukua taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu, isipokuwa utakapoamua kutupatia taarifa hizo.

Taarifa Inayochukuliwa

Unapotembelea Tovuti ya Muungano, Serikali tunaweza kuhifadhi baadhi ya taarifa zikiwemo anwani ya intaneti unakopitia, tarehe, muda, anwani ya Intaneti ya tovuti ulikounganishwa kwenye Tovuti ya Muungano, jina na kurasa ulizovinjari. Taarifa inayochukuliwa inatumika kubainishia idadi ya watu waliotumia sehemu mbalimbali za tovuti yetu na kubainisha maeneo yenye matatizo. Aidha, tunatumia taarifa hii kuboresha na kuifanya tovuti kuwa na manufaa zaidi. Tovuti ya Muungano inaweza kutumia taarifa hii pia kwa ajili ya uchambuzi wa utafiti.

Taarifa Binafsi

Taarifa zako binafsi hazitachukuliwa kwa madhumuni yoyote zaidi ya kushughulikia maombi yako. Taarifa inayojazwa kwenye fomu ya maoni itatumika tukujibu ujumbe wako, kusaidia kupata taarifa uliyoomba. Taarifa unayotupatia inaweza kupatiwa Taasisi nyingine ya Serikali iwapo swali lako linataihusu Taasisi hiyo, au vinginevyo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Matukio yajayo

22

Mar

Fainali za Mashindano ya Tamasha la Muziki.

24

Apr

Fainali za Kombe la Muungano

25

Apr

Mkesha wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

26

Apr

Sherehe za Kilele cha Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar